Nafasi za Kazi Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II (Nafasi 3,945), Nafasi za Kazi Assistant Nursing Officer Grade II, Ajira mpya za Assistant Nursing Officer
Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi 3,945 za Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II. Hii ni fursa kubwa kwa wataalamu wa fani ya uuguzi kujiunga na utumishi wa umma na kutoa huduma muhimu katika sekta ya afya nchini.
Majukumu ya Kazi Mtu atakayeajiriwa atakuwa na majukumu yafuatayo:
- Kutoa huduma za uuguzi.
- Kukusanya takwimu muhimu za afya.
- Kuwaelekeza kazi wauguzi walio chini yake.
- Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya.
- Kutoa huduma za kinga na uzazi.
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake.
Sifa za Mwombaji
- Mwombaji awe amehitimu kidato cha nne/sita.
- Awe na Stashahada (Diploma) ya Uuguzi ya muda usiopungua miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
- Awe amesajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.
Ngazi ya Mshahara
- TGHS B
Jinsi ya Kuomba na Masharti ya Jumla
- Mwisho wa Maombi: Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni 29 Oktoba, 2025.
- Mfumo wa Maombi: Maombi yote lazima yatumwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) unaopatikana kwa anwani: https://portal.ajira.go.tz/. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu huu hayatafikiriwa.
- Viambatisho Muhimu: Waombaji wote wanapaswa kuambatanisha CV yenye taarifa za kutosha, nakala za vyeti vya taaluma na cheti cha kuzaliwa vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Uraia na Umri: Waombaji wote lazima wawe Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45, isipokuwa kwa wale walioko tayari kazini serikalini.
- Kumbuka: “Testmonials”, “Provisional Results”, na “Statement of results” HAVITAKUBALIWA.