Nafasi za Kazi Mwalimu Daraja la IIIA (Nafasi 3,018), Nafasi za Kazi Teacher Grade IIIA: 3,018 positions, Ajira mpya za Teacher Grade IIIA
Katika jitihada za kuimarisha sekta ya elimu nchini, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, imetangaza nafasi 3,018 za Mwalimu Daraja la IIIA. Hii ni fursa adhimu kwa walimu wenye sifa kujiunga na utumishi wa umma na kuchangia katika kuwajenga viongozi wa baadaye wa taifa.
Majukumu ya Kazi Mwalimu Daraja la IIIA atawajibika na shughuli zifuatazo:
- Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi.
- Kutengeneza na kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia.
- Kufundisha, kufanya tathmini na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya wanafunzi.
- Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi shuleni na darasani.
- Kusimamia malezi ya wanafunzi kiakili, kimwili, kiroho na kutoa ushauri nasaha.
- Kusimamia utunzaji wa vifaa na mali za shule.
- Kufundisha na kusimamia Elimu ya Watu Wazima.
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule.
Sifa za Mwombaji
- Mwombaji awe na Cheti cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne.
- Awe amefaulu mafunzo ya Ualimu ya miaka miwili (2) kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambuliwa na Serikali na kutunukiwa Cheti cha Ualimu Daraja la A.
Ngazi ya Mshahara
- TGTS-B
Jinsi ya Kuomba na Masharti ya Jumla
- Mwisho wa Maombi: Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni 29 Oktoba, 2025.
- Mfumo wa Maombi: Maombi yote lazima yatumwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) unaopatikana kwa anwani: https://portal.ajira.go.tz/. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu huu hayatafikiriwa.
- Viambatisho Muhimu: Waombaji wote wanapaswa kuambatanisha CV yenye taarifa za kutosha, nakala za vyeti vya taaluma na cheti cha kuzaliwa vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Uraia na Umri: Waombaji wote lazima wawe Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45, isipokuwa kwa wale walioko tayari kazini serikalini.
- Kumbuka: “Testmonials”, “Provisional Results”, na “Statement of results” HAVITAKUBALIWA.