Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Uchaguzi Mkuu 2025 Yatolewa na Halmashauri Mbalimbali
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kupitia kwa Wasimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri mbalimbali nchini, imeanza kutoa orodha ya majina ya waombaji walioitwa kwenye usaili kwa ajili ya kazi za muda zitakazohusiana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Majina haya yanajumuisha watakaoshiriki kama Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo, Makarani Waongozaji wa Wapiga Kura, na nafasi nyingine muhimu.
Waombaji walioomba nafasi hizi katika Halmashauri na Majimbo mbalimbali wanashauriwa kufuatilia matangazo haya kwa makini ili kujua kama wamechaguliwa na pia kupata taarifa muhimu kuhusu tarehe, mahali, na saa za usaili.

Orodha ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili – Uchaguzi Mkuu 2025 (PDF)
Hapa chini ni jedwali la baadhi ya halmashauri na majimbo ambayo yametoa orodha za majina ya walioitwa kwenye usaili kwa ajili ya kazi za muda za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) 2025.
Na. | Jina la Halmashauri/Jimbo | Kiungo cha Kupakua Orodha (PDF) |
1. | Halmashauri ya Rombo | |
2. | Manispaa ya Bukoba Mjini | |
3. | Manispaa ya Newala Mjini | |
4. | Halmashauri ya Lindi Mjini | |
5. | Jimbo la Dodoma Mjini | |
6. | Wilaya ya Kisarawe | |
7. | Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo | |
8. | Jimbo la Lulindi na Ndanda | |
9. | Jimbo la Mbeya Vijijini | |
10. | Jimbo la Mtumba | |
11. | Halmashauri ya Mbulu | |
12. | Musoma Vijijini | |
13. | Wilaya ya Nkasi | |
14. | Wilaya ya Korogwe | |
15. | Pangani | |
16. | Kilosa | |
17. | Jimbo la Hai | |
18. | Jimbo la Kasulu Vijijini | |
19. | Mtwara Mjini | |
20. | Tabora Mjini | |
21. | Mkuranga | |
22. | Buhigwe | |
23. | Kibaha Vijijini | |
24. | Kibiti | |
25. | Nanyamba | |
26. | Same Magharibi | |
27. | Lushoto | |
28. | Gairo | |
29. | Babati | |
30. | Mafia |
Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa
Wasailiwa wote wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:
- Vyeti Halisi: Fika na vyeti vyako vyote halisi (original certificates) vya masomo na cheti cha kuzaliwa.
- Kitambulisho: Ni lazima uwe na kitambulisho kinachotambulika kisheria kama vile Kitambulisho cha Taifa (NIDA), Leseni ya Udereva, au Pasi ya Kusafiria.
- Picha: Fika na picha mbili za “passport size” za hivi karibuni.
- Muda: Zingatia tarehe na saa ya usaili kama ilivyoainishwa kwenye tangazo la Halmashauri yako. Kuchelewa kunaweza kusababisha ukose fursa ya kufanya usaili.
- Gharama: Serikali haitahusika na gharama zozote za usafiri, chakula, au malazi kwa watakaoitwa kwenye usaili.
Kwa taarifa zaidi na za uhakika, waombaji wanashauriwa kuendelea kufuatilia tovuti rasmi za Halmashauri walizoomba na mbao za matangazo katika ofisi za serikali za mitaa.