Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na JKT 2025 Yametoka!
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza rasmi majina ya vijana waliohitimu kidato cha sita mwaka 2025 walioteuliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka huu. Tangazo hili limekuja na wito wa Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, ambaye amewaalika vijana wote waliomaliza kidato cha sita kuhudhuria mafunzo haya ya kujenga uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, na utayari wa kulitumikia taifa.
Makambi ya JKT 2025
Vijana walioteuliwa wamepangiwa makambi mbalimbali nchini, ikiwemo:
- JKT Rwamkoma (Mara)
- JKT Msange (Tabora)
- JKT Ruvu na Kibiti (Pwani)
- JKT Mpwapwa na Makutupora (Dodoma)
- JKT Mafinga (Iringa)
- JKT Mlale (Ruvuma)
- JKT Mgambo na Maramba (Tanga)
- JKT Makuyuni na Orjolo (Arusha)
- JKT Bulombora, Kanembwa na Mtabila (Kigoma)
- JKT Itaka (Songwe)
- JKT Luwa na Milundikwa (Rukwa)
- JKT Nachingwea (Lindi)
Kwa wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities), wametakiwa kuripoti katika Kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi, Mkoani Pwani, ambayo ina miundombinu ya kuwahudumia.
Vifaa Vinavyohitajika
Vijana wanaotakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 28 Mei 2025 hadi 8 Juni 2025 wanapaswa kwenda na vifaa vifuatavyo:
- Bukta ya rangi ya Dark Blue yenye mpira kiunoni, isiyo na zipu, yenye mfuko mmoja nyuma, na urefu hadi magotini.
- T-shirt ya rangi ya kijani.
- Raba za michezo za rangi ya kijani au bluu.
- Shuka mbili za kulalia za rangi ya bluu bahari.
- Soksi ndefu za rangi nyeusi.
- Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
- Track suit ya rangi ya kijani au bluu.
- Nyaraka za udahili wa elimu ya juu (k.v. cheti cha kuzaliwa, vyeti vya kidato cha nne, n.k.).
- Nauli ya kwenda na kurudi makambini.

Jinsi ya Kuangalia Majina
Ili kujua kambi ambayo kijana amepangiwa, unahitaji:
- Kuingia kwenye tovuti rasmi ya JKT: www.jkt.mil.tz.
- Ingiza jina la shule au namba ya shule ambayo kijana alihitimu kidato cha sita.
- Bofya neno “Waliochaguliwa” linaloonekana mbele ya jina la shule. Hapa utaona majina ya vijana walioteuliwa, kambi waliyopangiwa, pamoja na mkoa na wilaya ya kambi hiyo.
- Kwa orodha kamili ya majina, pakua faili ya JKT PDF 2025 inayopatikana juu kulia kwenye ukurasa wa tovuti.
Wito wa Mkuu wa JKT
Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele amewakaribisha vijana wote waliomaliza kidato cha sita kujiunga na mafunzo haya ili kujifunza stadi za maisha, kujengewa uzalendo, na kuwa tayari kulijenga na kulitumikia taifa lao. Mafunzo haya ni fursa ya kipekee ya kukuza umoja wa kitaifa na kujifunza stadi za kazi zinazoweza kuwasaidia katika maisha yao ya baadaye.
Jitayarishe Sasa!
Ikiwa wewe ni miongoni mwa wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2025, hakikisha umejiandaa na vifaa vinavyohitajika na uangalie kambi uliyopangiwa kupitia tovuti rasmi ya JKT. Usikose fursa hii ya kujenga mustakabali wako na kuchangia maendeleo ya taifa lako!
Chanzo: Taarifa rasmi ya JKT, 27 Mei 2025.
Link ya Majina: www.jkt.mil.tz