Wanafunzi wa Kidato cha Sita Waliochaguliwa JKT 2025/2026, Orodha Yametoka!
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza rasmi orodha ya wanafunzi wa kidato cha sita waliomaliza mwaka 2025 walioteuliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2025/2026. Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, amewaalika wahitimu wote wa 2025 kutoka shule za Tanzania Bara kushiriki katika mafunzo haya ya kujenga uzalendo, umoja wa kitaifa, na stadi za maisha.
Maelezo ya Kuripoti
Vijana walioteuliwa wanatakiwa kuripoti makambini waliyopangiwa kuanzia 28 Mei 2025 hadi 8 Juni 2025. Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho wametakiwa kuripoti katika Kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi, Mkoani Pwani, ambayo ina miundombinu ya kuwahudumia.
Makambi ya JKT
Vijana wamepangiwa makambi mbalimbali nchini kama inavyoonekana kwenye jedwali hili:
Mkoa | Makambi ya JKT |
---|---|
Mara | Rwamkoma |
Tabora | Msange |
Pwani | Ruvu, Kibiti |
Dodoma | Mpwapwa, Makutupora |
Iringa | Mafinga |
Ruvuma | Mlale |
Tanga | Mgambo, Maramba |
Arusha | Makuyuni, Orjolo |
Kigoma | Bulombora, Kanembwa, Mtabila |
Songwe | Itaka |
Rukwa | Luwa, Milundikwa |
Lindi | Nachingwea |
Vifaa Vinavyohitajika
Vijana wanatakiwa kuleta vifaa vifuatavyo makambini:
Kifaa | Maelezo |
---|---|
Suruali | Rangi ya bluu dark blue, mpira kiunoni, urefu hadi magotini, mfuko mmoja nyuma, bila zipu |
Jezi | Rangi ya kijani |
Viatu vya Michezo | Rangi ya kijani au bluu |
Shuka za Kulalia | Mbili, rangi ya bluu bahari |
Soksi | Ndefu, rangi nyeusi |
Nguo za Kuzuia Baridi | Kwa mikoa yenye baridi |
Tracksuit | Rangi ya kijani au bluu |
Nyaraka za Elimu | Cheti cha kuzaliwa, vyeti vya kidato cha nne, n.k. |
Nauli | Ya kwenda na kurudi makambini |
Jinsi ya Kuangalia Majina
Ili kujua kambi uliyopangiwa:
- Tembelea tovuti rasmi ya JKT: www.jkt.mil.tz.
- Ingiza jina au namba ya shule uliyohitimu kidato cha sita.
- Bofya neno “Waliochaguliwa” ili kuona majina, kambi iliyopangiwa, na eneo lake.
- Pakua faili ya JKT PDF 2025 iliyopo juu kulia kwenye tovuti kwa orodha kamili.
Kwa Nini JKT ni Muhimu?
Mafunzo ya JKT ni fursa ya kipekee kwa vijana:
- Kujengewa uzalendo na umoja wa kitaifa.
- Kupata stadi za kazi na maisha.
- Kujiandaa kulitumikia na kulijenga taifa.
Meja Jenerali Mabele anawasihi vijana walioteuliwa kuchangamkia fursa hii ya kujifunza na kuchangia maendeleo ya Tanzania.
Jiandae Sasa!
Ikiwa wewe ni mwahitimu wa kidato cha sita mwaka 2025, angalia jina lako kwenye tovuti rasmi ya JKT, jitayarishe na vifaa vinavyohitajika, na ujiunge na safari hii ya kujenga mustakabali wako na taifa lako!
Chanzo: Taarifa Rasmi ya JKT, 27 Mei 2025
Link Rasmi ya Majina: www.jkt.mil.tz